Mshambuliaji wa Pyramids FC ya Misri, Fiston Mayele akifanya mahojiano na kituo cha habari cha Azam, ameeleza kuwa kocha aliyemkuta ndani ya kikosi cha Pyramids wakati anatokea Yanga Sc alitaka kumtoa kwa mkopo Disemba 2023 lakini Rais wa Klabu hiyo alizuia jambo hilo na kumuondosha kocha huyo.
“Wakati nakuja Pyramids kocha niliyemkuta alikuwa na wachezaji wake, na mimi nikaingia kuna wakati alinichezesha nilikuwa natoa assist au nafunga najua mechi hii nimefanya vizuri hivyo mechi ijayo nitaanza, mechi inakuja ananiweka tena nje.
“Ulifika wakati nikaenda kuongea na viongozi wa timu nikawaambia sikuja Pyramids kukaa nje kama mnaona mnaniweka nje Disemba (Disemba 2023) naondoka, niliwaambia hapa nimekuja kucheza.
“Disemba tulienda kucheza Kombe la Uarabuni na tukafungwa, baada ya ile mechi yule kocha akaandika list ya wachezaji wakutolewa kwa Mkopo jina langu lilikuwa la kwanza kwenye list, Rais wa timu akamwambia sawa tutakujibu.
“Mimi nikiwa AFCON yule Rais akanipigia akaniambia jina lako limetolewa huku utolewe kwa mkopo lakini siwezi kukubali kwasababu naamini utaisaidia timu yangu akaniambia mimi nitamuondoa yeye (Kocha), Rais akamuondoa yule kocha,” Mayele.