Mtangazaji wa michezo wa kituo cha radio cha Clouds FM, Alex Luambano amesema kuwa tatizo lililopo Simba SC kwa sasa ni mwekezaji wao Mohammed Dewji 'Mo' kwani ameshindwa kutoa pesa kwa ajili ya usajili na uendeshaji wa mambo mbalimbali ya timu na na kuitelekeza timu kwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo.
Luambano amesema hiyo ndiyo sababu kubwa ya Simba SC kuyymba na kupata matokeo mabovu ikiwemo kuishia robo fainali ya CAFCL, na robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB Bank na kwamba mwekezaji huyo hataki wawekezaji wengine wawekeze ndani ya Simba.
"Kuna watu wanataka kuwekeza Simba lakini Mo ni kikwazo, wanashindwa kwa sababu Mo amemiliki kila kitu, hivyo basi wamwambie afungue milango wengine nao waingie au atie hela akishindwa aachie kabisa.
"Hiki ninachozungumza kama kuna mjumbe wa bodi anaweza kuja kukanusha namkaribisha aje akanushe kwenye kipindi mbele yangu," amesema Luambano.