Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa tuhuma za kusambaza picha za ngoni

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa tuhuma za kusambaza picha za ngoni

 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu wawili akiwamo mpwa wa Hayati John Magufuli, Furaha Domic kwa tuhuma za kuratibu mtandao wa uhalifu wa kusambaza picha za ngono kwa lengo la kujipatia pesa.


Akizungumza na waandishi wa Habari jana Jumatatu jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum- SACP Jumanne Muliro amesema watu hao walikuwa wakisambaza picha hizo huku wakiwatisha wahusika ili kujipatia fedha.


Aliwataja watu hao ni; ”Furaha Dominic Jacob (32) mkazi wa Masaki na Mustapha Kihenge (28) Mkazi wa Mwenge TRA, wanatuhumiwa kutenda makosa ya uhalifu wa kimtandao. Wanadaiwa kusamba picha chafu za video za watu sizizo na maadili kwa lengo la kujipatia fedha kwa njia za vitisho.


“Watuhumiwa wote wawili watafikishwa mahakamani leo  Jumanne ili kukabiliana na tuhuma hizi,” alisema Muliro.


Furaha Dominic Jacob ambaye alikuwa mmoja wa makada wa CCM waliokuwa wameomba ridhaa ya chama hicho katika mbio za ubunge – Kawe kwenye uchaguzi wa mwaka 2020, alishinda kura za maoni lakini akaenguliwa na Rais Magufuli ambaye alikuwa mwenyekiti wa CCM.


Furaha alishinda kura za maoni ndani ya CCM kwa kupata  kura 101, Angela Kizigha alipata kura 85, Askofu Josephat Gwajima kura 79, Benjamin Sitta kura 61 na Vicent Mashinji ambae alihama CHADEMA na kwenda CCM aliibuka na kura 2.


Mwaka juzi Furaha alihojiwa na kituo cha runinga cha Star Tv na alielezea namna hayati Magufuli alivyokuwa amezungukwa na watu aliodai ni waongo, wazushi na wafitini (kupe) waliosababisha wakati mwingine afanye maamuzi yasiyo sahihi yaliyoumiza wasio na hatia.


Alidai watu hao walimuwekea zengwe hadi akaukosa ubunge wa Kawe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad