Taarifa ya mamlaka ya hali ya hewa iliyotolewa kupitia vyombo vya habari nchini, imetoa angalizo la kutokea kwa mvua katika kipindi cha siku tano, huku ikifafanua kuwa kiwango cha athari zinazoweza kujitokeza ni za Wastani.
Kulingana na taarifa hiyo ya TMA, hali mbaya ya hewa itakayoambatana na mvua pamoja na ngurumo za hapa na pale inatazamiwa kutokea kwenye mikoa zaidi ya 10 ikiwemo Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Lindi, Mtwara pamoja na Visiwa vya Pemba na Unguja.
"Kwenye mikoa hiyo kunatarajiwa kuwepo na hali ya Mawingi, Mvua, ngurumo kwenye baadhi ya maeneo na vipindi vifupi vya Jua" imeeleza Ripoti hiyo ya TMA.
Wakati huo huo Mamlaka hiyo imetoa tahadhari ya Upepo ya Upepo mkali unazidi kilomita 40 kwa Saa pamoja na Mawimbi makubwa yanazidi mita 2 kweny ukanda wa maeneo ya Pwani ya Bahari ya Hindi.
Sanjari na hayo mamlaka ya hali ya hewa TMA imewataka Wananchi kwenye mikoa hiyo kuchukua tahadhari kwa Sababu mvua hizo zinaweza kusababisha Makazi kuzunguukwa na maji na kusimama kwa muda Shughuli za Kiuchumi, ikiwemo Uvuvi na Usafirishaji Baharini.