Pamoja na Kuifunga Jana SIMBA Kocha Gamondi Bado Haamini Kuwa Ubingwa ni wao

 

Pamoja na Kuifunga Jana SIMBA Kocha Gamondi Bado Haamini Kuwa Ubingwa ni wao

Pamoja na Kuifunga Jana SIMBA Kocha Gamondi Bado Haamini Kuwa Ubingwa ni wao

Kocha Mkuu wa Young Africans SC, Miguel Gamondi, amefunguka kwamba, suala la ubingwa kwa sasa ni mapema kuzungumzia, licha ya kwamba tuna nafasi kubwa ya kubeba.


Kauli ya Gamondi imekuja baada ya kushinda kwa magoli 2-1 dhidi ya Simba na kufikisha pointi 58, huku tukibakiwa na michezo nane ambayo tukishinda sita pekee, ubingwa wetu.


“Katika maisha usiweke kitu kujiaminisha sana, bado tuna mechi za kucheza, ni kweli tuna gepu kubwa, lakini tunapaswa kucheza.


“Unafahamu falsafa yangu ni hatua kwa hatua, kwa sasa tumepiga hatua kubwa, lakini usisahau Jumanne tuna mechi nyingine na Jumamosi mechi nyingine, kila timu inataka kufanya kitu dhidi yetu, hivyo itakuwa ngumu.”


Baada ya jana, katika muendelezo wa Ligi Kuu ya NBC, Jumanne ya Aprili 23 tutakuwa ugenini kupambana na JKT Tanzania, kisha Jumamosi ijayo tutacheza nyumbani dhidi ya Coastal Union.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad