Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema kwake uongozi ni suala la kuacha alama na sio ni muda gani amehudumu katika uongozi huo.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kutoka kwa mtangulizi wake John Mongella, Makonda amesema anajivunia kufanya ziara ya kikazi katika mikoa 25 licha ya kuhudumu kwa miezi mitano tu kama Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Yani hapa nilipo naona kama nimechelewa ilibidi saa hizi niwepo site (kazini),” amesema Makonda.
Amesema kwake, kipaumbele chake ni kujitoa, kuchapakazi, kutatua changamoto za wananchi.
“Nitabadilika kutokana na mahitaji yenu. Mkitaka Arusha uwe mji ambao mtu akiangusha simu yake anaitiwa. Mkitaka Barabara zipitike itakuwa,” amesema Makonda.