Refa Aliyekataa Bao la Aziz Ki Apewa Shavu na FIFA

 

Refa Aliyekataa Bao la Aziz Ki Apewa Shavu na FIFA

Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limemteua refa Beida Dahane aliyechezesha mechi ya Mamelodi na Yanga, ljumaa iliyopita kuchezesha mechi za soka za mashindano ya Olimpiki itakayofanyika Ufaransa kuanzia Julai 26 hadi Agosti 11, mwaka huu.


Dahane (32) ni miongoni mwa marefa 12 kutoka Afrika ambao wamepata fursa hiyo huku kiujumla wakiteuliwa marefa 89 kutoka nchi tofauti duniani.


Marefa kutoka Afrika walioteuliwa kuchezesha Olimpiki mwaka huu ni walioteuliwa kuchezesha michezo ya Olimpiki mwaka huu ni Karboubi Bouchraw wa Morocco, Mahmood Ismail(Sudan), Diana Chkotesha(Zambia), Fatiha Jermoumi(Morocco), Elvis Noupue (Cameroon), Stephen Yiembe.


(Kenya), Mahmoud Ashour (Misri), Lahlou Benbraham (Algeria), Ahmed Abdoulrazack (Djibouti), Emiliano Dos Santos (Angola) na Shamirah Nabadda Uganda).


ljumaa iliyopita Dahane alizua mjadala baada ya kukataa bao la kiungo wa Yanga, Stephane Aziz Ki ambalo kwa mujibu wa baadhi ya picha za video na za mnato, mpira ulivuka wote mstari wa goli ingawa kwa uamuzi wa refa, haukuvuka wote.


Katika mchezo huo Yanga iliondolewa kwenye hatua ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa penalti 3-2.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad