Shaffih Dauda: Simba Bado Haijatoka Kwenye MBIO za Ubingwa, Acheni Kuongea Sana


Simba haijafanya vibaya kama ambavyo inazungumzwa, imetolewa kwenye Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ambayo imekuwa kikwazo kwao kwa misimu kadhaa mfululizo.

Kwenye makombe ya nyumbani imetolewa CRDB Bank Federation Cup hatua ya 16 bora, Simba tangu iliponyang’anywa kombe hili bado inapigana kulirudisha.

Simba bado inanafasi ya kuchukua Kombe la Ligi Kuu, hesabu za kwenye makaratasi bado zinakubali/zinaonesha nafasi ya Simba kuwa bingwa.

Hadi sasa Yanga ipo mbele ya Simba kwa alama tisa [9], timu hizo zinakutana Jumamosi kwenye mechi ya Ligi, Simba ikifanikiwa kushinda maana yake tofauti inabaki alama sita [6].

Simba ina mchezo mmoja wa kiporo dhidi ya Azam FC, ikiwa Simba itashinda mchezo huo maana yake inakuwa imeipunguza kasi Azam FC kwenye mbio za ubingwa lakini tofauti ya alama dhidi ya Yanga itakuwa imebaki tatu.

Kwa hiyo kwenye makaratasi Simba bado haijatoka kwenye mbio za ubingwa lakini ukiwasikiliza mashabiki tayari morali ipo chini na wamekata tamaa.

Mashabiki wa Simba wanapaswa kuwa waungwana na wanamichezo, kabla ya Yanga kuingia na kutawala soka la nyumbani wao walitawala kwa misimu minne mfululizo. Yanga kama watachukua msimu huu itakuwa ni mara yao ya tatu mfululizo kwa misimu ya hivi karibuni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad