Shaffih Dauda: Simba Wakubali Msimu Umeisha Wapiganie Nafasi ya pili




1.NJE YA UWANJA

Kwanza nimefurahi kuona kelele za mashabiki wa Simba sio nyingi kama ambavyo ilikuwa hapa kati kati , ni ishara kuwa tayari wamekubali kuwa hawana timu bora msimu huu .

Hii ni hatua ya kuanzia kwenye kujenga timu ini lazima kwanza ukubali hali ya timu yako , hakuna uongo wowote ambao mashabiki wa Simba wanataka kusikia kwa sasa.

Walishinikiza uongozi upishe lakini shinikizo halijazaa matunda , Viongozi waliopo kama wataendelea kuwepo wawatafutie furaha ya uhakika hawa mashabiki ambao kelele zao zinaqnzia kwa hao hao viongozi .

2.KIUFUNDI

Simba SC imecheza michezo 21 ya Ligi kuu hadi sasa kati ya mechi 30 , kimahesabu amebakisha mechi 9 ambazo ni sawa na alama 27 ,alama ambazo zinaweza kubadili chochote na kumfanya kuwa bingwa kama ambavyo viongozi wao wamekuwa wakiwaambia mashabiki wao

Lakini kwa form ya Yanga ni ngumu hiko kutokea , Simba wakubali kuwa msimu umeisha kilichobaki ni kupigania nafasi ya pili ili washiriki Champions League msimu ujao .

Kwa upande wa wachezaji ni muda sasa wq kila anayelipwq na simba kuanza kupewa dakika ili kuona je 2024/25 ataendelea kuwepo au apishe nafasi wapewe wengine .

Wapo wachezaji wa kikosi cha kwanzq cha Simba hawashawishi kabisq kuwaangalia nafikiri hao hawana cha kubadilisha kwa mechi 9 , Viongozi wafanye maamuzi magumu na wakifanya hivyo kile kikosi cha kwanza wanaweza kubaki sio zaidi ya wachezaji wanne .

DIGALA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad