Simba Kutolewa na Mashujaa, Shida ya Wachezaji wa Simba Ipo Kichwani


Nilichokiona Kigoma nilikitarajia kutokana na mechi mbili za Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa ambazo Simba imetoka kucheza dhidi ya Al Ahly.

Muda ambao Simba walipata kwenda Kigoma, saikolojia ya wachezaji kutoka kupoteza mchezo wa Ligi ya Mabingwa kuirudisha kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa, mwalimu anakuwa na kazi kubwa sana kutengeneza morali ya wachezaji.

Kuna watu wanaweza kusema wachezaji kazi yao ni kucheza lakini mwisho wa siku kichwa ndio kinafanya kazi, kama mchezaji hayupo sawa kichwani hawezi kutoa kile ambacho kinatarajiwa.

Kwa kiwango kilichooneshwa na Simba kwenye mechi mbili dhidi ya Al Ahly, hata shabiki wa kawaida alitarajia kuona Mashujaa wanafungwa na Simba.

Sisi ambao tupo kwenye tasnia tulikuwa tunatarajia mechi ngumu sana kutokana na uchovu wa Simba na kile ambacho walikuwa wanatarajia kukipata dhidi ya Al Ahly halafu wakapoteza.

Ilikuwa ni ngumu kuona wachezaji wa Simba wakicheza dhidi ya Mashujaa kwa hamasa na kujitoa kama ilivyokuwa kwenye michezo miwili dhidi ya Al Ahly.

- Mkongwe Amri Kiemba kuhusu Simba kutolewa na Mashujaa FC

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad