Simba Vs Al Ahly, Serikali Yasikiliza Kilio cha Mashabiki wa Simba

Simba Vs Al Ahly, Serikali Yasikiliza Kilio cha Mashabiki wa Simba



Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’ amesema, mara baada ya serikali kusafirisha mashabiki 48 wa Yanga kwenda Afrika Kusini, klabu ya Simba imetuma maombi kuomba ndege ili iwasafirishe mashabiki wake kwenda kuishangilia timu yao nchini Misri.

“Tumewaaga wapenzi 48 wa Yanga ambao wamesafiri kwa njia ya barabara kwenda Afrika Kusini kushuhudia mchezo wa marudiano wa Mamelodi Sundowns dhidi ya Yanga.”

“Baada ya jambo hilo, klabu ya Simba nayo imeleta maombi yake ambayo tunayashughulikia na ninaamini wapenzi wa Simba pia watapata fursa ya kwenda kushuhudia mechi ya marudiano ya Al Ahly dhidi ya Simba.”

“Ni jambo la kiutaratibu, klabu inatakiwa iseme inataka nini halafu serikali tutaona kama lipo ndani ya uwezo wetu kwa wakati huo na tunayafanya. Kama ambavyo tulifanya kwa klabu ya Yanga, maombi ya klabu ya Simba tumeyapokea na tunayafanyia kazi.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad