Taarifa ya Jeshi la Polisi Kuhusu Kifo Cha Zuchy, Mpiga Picha wa Ayo TV



Kuna taarifa yenye kichwa cha habari SHUHUDA inayosambazwa katika mitandao ikieleza

“Zuchy kapata ajali na boda hit and run mbele ya mataa ya masana kama 100 mita hivi toka saa nane usiku dereva wa boda akapelekwa hospital. Umoja wa bodaboda wamekaa na mwili barabarani pale wakiita Polisi kisingizio gari haina mafuta kweli. Pia tarifa hiyo inaeleza bodaboda walikaa na mwili hadi wakafunga barabara ili kushinikiza Polisi waitwe.”

Kwanza, Jeshi la Polisi linasema hili ni tukio la huzuni na la kusikitisha kwasababu tumempoteza Mtanzania mwenzetu katika ajali hiyo.

Pia lingependa kueleza kuwa, tukio hilo liliripotiwa saa kumi na dakika kumi na mbili alfajiri kuwa, kuna ajali imetokea eneo la Mbezi Makonde. Baada ya kupokelewa tarifa hiyo Maafisa na Askari waliokuwa kwenye majukumu katika mkesha wa Tamasha la Shangwe la Utawala lililokuwa linafanyika eneo la Tanganyika Packers waliondoka wakiwa na gari ya Polisi kuelekea eneo la tukio na kuchukuwa mwili wa marehemu na kuupeleka Hospitali ya Mwananyamala kwa taratibu zingine za kisheria.

Askari waliofika eneo la tukio katika uchunguzi imebainika marehemu alipata ajali na pikipiki aliyokuwa amepanda yenye namba MC 436 CMU iliyokuwa ikiendeshwa na dereva ambaye
alipata majeraha na anaendelea na matibabu.

Hivyo, mara baada ya tarifa ya tukio hilo kutolewa na kupokelewa, Maafisa na Askari Polisi walifika kwenye tukio kwa wakati na kutekeleza yale yanayopaswa kutekelezwa kwenye eneo la ajali.

Tunawashukuru bodaboda wa eneo hilo wanaojali utu wa binadamu kwa kuzuia magari yasimkanyage marehemu.

Endapo kuna mwenye tarifa tofauti na si za uzushi/uwongo kama hizo zinazosambazwa azifikishe kwa viongozi ili zifanyiwe kazi na hatua zichukuliwe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad