Aliyewahi kuwa beki wa kulia wa klabu ya Yanga, Suleiman Abdallah Mkati amefariki dunia leo katika hospitali ya Temeke alipopelekwa kwa matibabu akiwa ana umri wa miaka 53.
Suleiman Abdallah Mkati aliyezaliwa Desemba 18, 1969, aliibukia katika klabu ya Sigara FC ambako alicheza kuanzia mwaka 1984 hadi 1989 akahamia Pilsner, zote za Dar es Salaam.
Alicheza Pislner hadi mwaka 1991 aliposajiliwa na vigogo wa soka nchini, Yanga SC ambako alidumu hadi mwaka 1995 aliporejea Sigara ambako alicheza tena hadi mwaka 1997.
Mwaka 1998 akachukuliwa na wa jina lake, Suleiman Mathew kwenda kuisaidia timu ya Mto ya Singida, baadaye Singida United 2000 kupanda Ligi Kuu na ilipopanda tu mwaka 1999 Mkati akastaafu soka.
Mkati ambaye pia alicheza timu ya taifa kuanzia mwaka 1989 hadi mwaka 1991 - baada ya kustaafu soka alipata mafunzo mbalimbali ya ukocha.