UCHAMBUZI: Yanga Wanashinda Back to Back Mbele ya Simba Msimu Huu


Yanga na Simba
Yanga na Simba

Mchezo ulikuwa na risk sana , ukidelay kidogo tayari upo nje ya move : uwanja ulikuwa unateleza sana …. Nini kilitokea baada ya kuonekana hivo ? Yanga walionesha ubora wao .

Yanga kama kawaida yao 4-2-3-1 , walianza mpira nyuma kwa shape ya 2-3-4-1 (Aucho mbele ya CBs wawili then Muda anasogea juu kuungana na Maxi , Aziz na Mzize nyuma ya Guede ) : Yanga waliitaji kuongeza kasi kwenye kushambulia tu .

1: Walipata nafasi kubwa sana nyuma ya kiungo cha Simba , Muda Aziz na Maxi walishambulia vizuri sana then ni Yanga tu , kwasababu walikuwa na runners wengi wakishambulia (Yao , Mzize , Kibabage) .

2: Nafikiri kwa zile Space walizokuwa wanazipata + Simba hawaweki presha ni wao tu , hawakuhitaji pasi nyingi kufika kwenye Defense ya Simba : Simba walikuwa hawaweki presha kwenye mpira na kwa mpinzani .

Simba kwa nafasi walizokuwa wanaziacha aisee : unauliza nini wanafanya kwenye uwanja wa mazoezi hasa wakiwa hawana mpira . Wapo wazi sana , hawaweki presha kwa mpinzani na kwenye mpira …. Ngoma , Babacar na Kanouté walikuwa wanapoteza pasi kirahisi sana then hawakuzuia vizuri .

Nafikiri baada ya kuingia kwa Fred , Luis …. Simba waliongeza uhai kwenye eneo la mbele (Movements , idadi ya wachezaji na waliisumbua Defense ya Yanga) …. Baada ya kuwa 2-1 Yanga waliamua kuzuia kwa kulinda alichonacho : ZUIA VIZURI .

NOTE:

Yule Aziz Ki “Very Technician” ukimuachia nafasi aisee upo hatarini🔥 ….. Job na Bacca 👏

Joseph Guedé “A Striker✅” amecheza game bora sana .

Chama na Che Malone ✅

Yanga wanashinda Back to Back mbele ya Simba msimu huu .

FT: Yanga 2-1 Simba .

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad