Usajili ni sanaa, usipokuwa mwelewa utasajili hovyop - Hersi

 

Usajili ni sanaa, usipokuwa mwelewa utasajili hovyop - Hersi

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema kuwa suala la usajili wa wachezaji linahitaji uelewa mkubwa la sivyo kama kiongozi wa Klabu unaweza kuishia kusajili wachezaji magarasa ambao hawatakusaidia kwenye kutimiza malengo ya timu.


Hersi amesema hayo wakati akizungumzia maamuzi yake ya kufanya usajili wa wachezaji yeye mwenyewe badala ya kutuma watu.


"Usajili ni sanaa, ni lazima ujue kwanini unafanya huo usajili. Kwa kifupi huwezi kubaki na wachezaji wako wazuri kwa muda wote, hivyo inabidi utengeneze mazingira mazuri ya kuvutia Wachezaji wengine wazuri. Hivyo nilichukua maamuzi ya kusimamia mchakato wa usajili.


"Unapokuwa Kiongozi lazima uwe na maono makubwa sana na uelewa mkubwa wa mpira. Unapaswa kujua mchezaji yupo kwenye kilele cha ubora wake, anapata wakati mgumu kuzuoea mazingira, amechoka nk. Usipokuwa na uelewa wa mpira basi utajikuta unasajili hovyo au unatimua wachezaji kwa hisia.


"Niliamua kuingia mwenyewe kwenye usajili ili kwenda moja kwa moja kuonana na wachezaji, kujenga uaminifu na kujua kiundani kuhusu wachezaji ninaowahitaji badala ya kutuma mtu ambaye angefanya tofauti na ninavyotaka iwe," amesema Hersi Said.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad