V8 Nyingine Yanaswa Iringa ikisafirisha wahamiaji haramu

V8 Nyingine Yanaswa Iringa ikisafirisha wahamiaji haramu


Jeshi la polisi mkoa wa Iringa limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 16 raia wa Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.


Akizungumza na vyombo vya habari mjini Mafinga jana Aprili 8, 2024, kamanda wa polisi mkoa wa Iringa hapa, Allan Bukumbi amesema jeshi hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Uhamiaji mkoani humo wamefanikiwa kuwakamata walhamiaji hao 16 raia wa Ethiopia katika eneo la msitu wa Luganga, kata ya Sao Hill, wilayani Mufindi.


Kamanda Bukumbi amesema wahamiaji hao haramu waliwakamata wakiwa wametelekezwa katika shamba la mahindi baada ya kushushwa kwenye gari ambalo awali lilikuwa likisomeka namba za usajili STL 3999 aina ya Land Cruiser V8 1lenye rangi nyeupe ambapo dereva wake alilitelekeza baada ya kuona anafuatiliwa na askari.


"Baada ya dereva huyo kuona anafuatiliwa na askari, akaona hataweza kupita barabara kuu, hivyo alipita njia nyingine na kufika sehemu ambako alikutana na tikiti (swap), hali iliyowafanya washindwe kuendelea na safari hiyo, ndipo alipowashusha wahamiaji hao na kuifunga na kutokomea kusikijulikana," amesema RPC Bukumbi.


Ameongeza kuwa uchunguzi wa awali umebaini kwamba gari hiyo imesajiliwa kwa namba T803 CVW linalomnilikiwa na Saidi Hassan, nmkazi wa Tabata, Dar es Salaam huku akieleza jitihada mbalimbali ambazo zinaendelea za kumtafuta dereva pamoja na mmiliki wa gari hilo.


Kwa upande wake, ofisa uhamiaji wa mkoa wa Iringa, Peter Kimario amesema biashara hiyo haramu ya binadamu ni mbaya kwani inahatarisha usalama wa Taifa hili.


"Kupitia vyombo vya habari, natoa wito kwa Watanzania watusaidie katika kampeni yetu ambayo imeanzishwa nchini mzima inayoitwa 'Mjue Jirani Yako' kwa sababu hawa tumewakamtwa kwenye magari ya aina hiyo, hivyo tunaamini wanaweza kutumia mbinu za kuvaa vizuri kama Watanzania na kusafiri katika vyombo vya usafiri vya kawaida bila kuwajua," amesema Kimario Kimario amefafanua kuwa kampeni hiyo ya mjue Jirani yako imeanzishwa ili kujua vitu ambavyo vinaendelea katika maisha ya wananchi kwa sababu usalamna wa nchi, kila mtu anahusika katika jambo hilo.


Hata hivyo, amesisitiza kuwa Jeshi la Uhamiaji litaendelea kushirikiana na vyombo vingine ili kuhakikisha wahamiaji hao wanafikishwa kwenye vyombo husika na kuchukuliwa hatua.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad