Wala Mo Dewji Sio Tatizo Simba, Pacome Mlimkataa Wenyewe Mkachukua Magarasa - Farhan

 

Mo Dewji sio Tatizo Simba, Pacome Mlimkataa - Farhan

1- MCHAKATO WA MABORESHO YA KIKOSI, leo hii timu imefika hapa ni ghafla sana MO DEWJl anatajwa kuwa ni tatizo kuwa hatoi pesa ndani ya timu ila kwanza tuzungumzie ripoti ya Kitalaam ambayo Simba mliipokea na mnaifahamu vyema, iliyokuwa inahusu mabadiliko ndani ya kikosi kwakuwa sehemu kubwa kimechoka.


Viongozi wa Simba kama nitakuwa naongea uongo mtatoka hadharani kunipinga nami nitaomba radhi! Taarifa za kiuchunguzi nilizonazoni kuwa baadhi ya Wachezaji na maeneo yao yalitajwa wanapaswa kupisha ili Wachezaji wapya waingie kikosini ila mkatia ngumu kutokana na kutowepo Watu wa kiufundi wala Kamati ya Usajili.


Saido Ntibazonkiza ni moja kati ya nyota ambao mliambiwa apishe kikosini na mkapokea mapendekezo ya majina ya nyota wanaopatikana kwa gharama nafuu kuliko Saido na mnachomlipa! Nawataja wachezaji hao ni PACOME ZOUZOUA, SIDI BOUNA, BRAHIMA OUTTARA na nyota mwingine wa Nigeria.


Mkaziba masikio na kutowachukua Wachezaji hawa wa bei rahisi, matokeo yake Pacome akasaini Yanga, Sidi nasikia yupo zake Wydad Athletic! Kama hamkupokea hii ripoti na kutoifanyia kazi hapo klabuni tafadhali mnifahamishe! Mpaka hapa sehemu ya kwanza MO anahusika vipi na yanayoendelea? Ikiwa best talents mkazikataa kwa gharama nafuu.


Mmeshawahi kuwaambia Wanasimba kuwa hata Striker OMAR JOBE hakuwa chaguo la mwanzo kwenye ripoti ya Mastreika ambao wanapaswa kucheza Simba? Mliwaambia kuwa BABACAR SARR ni usajili ambao haukupitishwa ila watu wachache mkaamua na ghafla akatangazwa kuwa ni Mchezaji wa Simba?


MO wanasema hatoi hela okay ila BENCHIKA ni Kocha moja wapo ghali zaidi hapa kwenye Ligi yetu, hamkupewa ABC kuwa ni Kocha anayetaka kufanya kazi na wachezaji wakubwa na wazoefu?


Hamkuambiwa uwezo wake na Wachezaji waliopo ni vitu viwili tofautí? Hamkuambiwa anahitajika Mkurugenzi wa Ufundi kwa ajili ya usajili na sio ninyi hapo juu kwakuwa mpira haupo hivyo?


2- MKUTANO MKUU, mlisema MO anatoa mzigo kupitia bidhaa zake na uwekezaji amefanya! Mkasema timu imetengeneza FAIDA na sio hasara! Mbona ghafla sana MO HATOl HELA? Hela which kwa timu inayozalisha faida? tulipangwa mkutanoni? Ni pesa ama ni mfumo wa Uongozi??


VIONGOZI WA SIMBA mliopo sasa mtanisahihisha kama kuna sehemu nadanganya nami nitakiri kosa, mnakumbuka moja kati ya mifumo ambayo mlikuta kwenye hii Simba ni mahusiano kati ya timu na timu, timu na shirikisho, timu na wafanyabiashara na timu dhidi ya Mawakala ama Kampuni za Uwakala.


Nataka tukae hapa kwenye RELATIONSHIP BETWEEN CLUB VS AGENCY, uhusiano kati ya klabu na Mawakala ama Kampuni za Mawakala, hii ndio sehemu ambayo ilipelekea timu ipate Wachezaji wengi bora sana kikosini, malipo mazuri ya commision kwa Mawakala na mifumo bora tulipata Mapro wakali sana rejea kumbukumbu.


Shida ilianza pale ambapo viongozi mkaanza kupishana na Mawakala pamoja na Kampuni zao, nikimtaja CHE MALONE mnakumbuka kisa chake, mliletewa jina na Mtanzania tu na alikuwa na link nae, mkamzunguka na ilibaki nusu mumkose Mchezaji alikuwa akasaini Singida kama sio busara za Agent mliomzunguka kumwomba Mwakilishi wa Mchezaji asaini Simba.


Sio ninyi Viongozi mliopo hapo madarakani mliletewa Pacome mpaka mlangoni, Ouattara yule Dogo mpaka mlangoni na kukosa kwetu Mtu mwenye jicho la Kiufundi hapo kwenye Uongozi ukatukosesha hizi talents, bila Watu wa Kiufundi na kuzingatia ushauri wa Watalaam mnahisi ni rahisi kupata talents?


Waambieni ukweli Wanasimba kuwa Yanga walipoipata ripoti ya Kitalaam kutoka kwa timu ya Mawakala na Kampuni ndipo wakapita mbele yenu kumnasa Pacome ambapo alitakiwa aje na Ouattara Brahima?


Kama sio Rais wa Shirikisho la soka la Ivory Coast kuingilia kati basi Yanga walikuwa wanashusha silaha zote mbili kwa pamoja, jitafakarini mmewaudhi Mawakala wengi wanabeba talents wanapeleka kwingine.


Timu imekosea kwenye usajili wala sio suala la MO DEWJI kutotoa pesa hiyo sio kweli, yule Mtoto HORSO MWAKU mliletewa hadi Mlangoni ni STRIKER wa maaana tena umri mdogo sana, nae tushangae mpaka asaini Yanga kisha tuje kulaumu kuwa MO hatoi hela? Timu imepoteza network yake na Mawakala ni ngumu kusogea.


Cha kwanza rudini kwenye script ya SENZO na BARBRA, rejesheni imaani ya Mawakala na Kampuni zao, watawaletea top talents ambazo ni gharama nafuu sana, tafuteni MKURUGENZI WA UFUNDI na KAMATI YA USAJILI wafanye kazi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad