Wanariadha Waliompisha Mchina kushinda Marathon wanyang'anywa Medali

 

Wanariadha Waliompisha Mchina kushinda Marathon wanyang'anywa Medali

Washindi watatu wa mbio za nusu marathon ya Beijing wamenyang’anywa medali zao kufuatia uchunguzi juu ya matokeo yaliyozua utata.


Ilituhumiwa kuwa wanariadha watatu kutoka Afrika walimuachia kwa makusudi mwanariadha wa China He Jie ashinde mbio za siku ya Jumapili.


Picha zilionesha wanariadha wa Kenya Robert Keter na Willy Mnangat pamoja na Dejene Hailu wa Ethiopia wakitoa ishara kwa mikono na kupunguza mwendo na kumuachia He apite.


Mnangat aliiambia BBC kuwa watatu hao walikuwa wakikimbia kama wachochea kasi.


Lakini kamati ya maandalizi iliyoongoza uchunguzi huo imesema hakuna kati ya hao watatu aliyekuwa ameandikishwa kama mchochea kasi wa He, na hivyo matendo yao yamekiuka sheria za mchezo.


Kamati hiyo imesema “medali zote na bakshishi walizopewa zitarejeshwa”.


Kituo cha habari cha CCTV kimeripoti kuwa wanariadha wote wanne “wameadhibiwa” na matokeo yao kufutwa.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad