Ahly, Zamalek watawala Kikosi cha Misri

Ahly, Zamalek watawala Kikosi cha Misri


Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Misri Hossam Hassan ametangaza kikosi cha wachezaji 25, kwa ajili ya michezo miwili ya kuwania Kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2026 itakayopigwa mapema mwezi ujao dhidi ya Burkina Faso na Guinea-Bissau itakayopigwa Juni 06 na 10.


Misri itaanzia nyumbani mjini Cairo kwa kuikaribisha Burkina Faso, kisha itasafiri kuelekea Guinea-Bissau.


Kocha Hossam ametaja kikosi chake, huku akiwajumuisha wachezaji watano wanaocheza nje ya Misri na waliosalia wanatoa kwenye Klabu Bingwa Barani Afrika Al Ahly, wengine wakitoka kwa Mabingwa wa Kombe la Shirikisho Zamalek.


Walinda Lango: Mohamed El Shenawy, Mostafa Shobeir, Mohamed Awad na El Mahdy Soliman.


Mabeki: Mohamed Abdel Moneim, Rami Rabia, Yasser Ibrahim, Mohamed Hany, Akram Tawfik, Ahmed Ramadan, Mohamed Hamdy na Ahmed Fatouh.


Viungo: Marwan Attia, Hamdi Fathi, Ahmed Nabil Koka, Emam Ashour, Ahmed Sayed Zizo, Nasser Maher, Mostafa Fathi, Mahmoud Trezeguet na Mohamed Salah.


Washambuliaji: Mostafa Mohamed, Mohamed El Shamy, Mohamed Sherif na Ahmed Amin Oufa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad