Ahmed Ally Arusha Kijembe Kwa Yanga: Mkimnunua Kibu Denis Mtafilisika

 

Ahmed Ally Arusha Kijembe Kwa Yanga: Mkimnunua Kibu Denis Mtafilisika

Meneja wa Habari na Mawasiliano na Msemaji wa Klabu wa Simba SC, Ahmed Ally amesema mchezaji wao Kibu Denis ambaye alihusishwa kujiunga na watani wao wa jadi Yanga hatoondoka klabuni hapo na ikiwa watataka kumnunua wajiandae kufilisika na kwamba suala la malipo kwao sio shida.


Ahmed Ameyasema hayo katika mahojiano maalum na Crown media akifananisha suala hilo na kulitoa jua Mashariki lichomoze magharibi.


“Wana hatari ya kufilisika hao hawana uwezo wa kumiliki mchezaji aina ya Kibu, hawana cha kumlipa Kibu Denis Prosper hawana uwezo wa kuchukua mchezaji Simba Sports Club niamini mimi. Haiwezi kutokea yani ni sawa na kulitoa jua Mashariki lichomoze magharibi,” amesema Ahmed.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad