“Nitashangaa kumuona uyu Mwalimu (Miguel Gamondi) kwenye tuzo ya Makocha bora msimu huu
Haijalishi ame-achieve nini lakini hastahili chochote kwa utovu wake wa nidhamu uliopitiliza.
“How come Mwalimu Mkuu unakuwa na tabia za hivyo?? Ina maana asingezuiliwa angepigana??
Vitendo hivi vinachafua mpira wetu na inaonekana ligi ya wahuni, wasio na ustaaarabu.
“Kama kila asieridhishwa na maamuzi afanye vurugu hii si itakuwa ligi ya kina Mwakinyo
Halafu hapo bado wapo kwenye mchezo Mwamuzi huyu alishindwa nini kumuonesha kadi nyekundu??
“Hii tabia ya Watu wa Nyuma Mwiko kuwafanyia vurugu Waamuzi imeota mizizi sasa hii tabia inapaswa kukomeshwa tena kwa haraka kwanza usalama wa Waamuzi wetu pili kulinda thamani na hadhi ya mpira wetu.
“Hatuko tayari kuona watu wachache wanachafua taswira ya mpira wetu na hawa nyuma mwiko lazima wakumbushwe kuwa hawapo juu ya sheria.
Ameandika, Ahmed Ally, Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba Sc kupitia mtandao wake wa Instagram.