Juma Mgunda Ndie Kocha Bora Tanzania Hivi Sasa...Ahmedy Ally Afunguka


Juma Mgunda Ndie Kocha Bora Tanzania Hivi Sasa...Ahmedy Ally Afunguka

Juma Mgunda ndie Kocha bora Tanzania hivi sasa


"Kocha Mgunda alianza msimu akiwa na timu ya Simba Queens na ameiwezesha timu hiyo kutwaa Ubingwa akiwa hajapoteza mechi hata moja

Baada ya kuipa Ubingwa Queens, sasa yupo Simba Senior team na amefanya mabadiliko makubwa kwenye timu

Ameweza kunyanyua viwango vya Wachezaji na ataiwezesha Simba kumaliza nafasi mbili za juu

Ni Kocha mwenye uwezo wa kuzalisha, kutengeneza na kuendeleza kipaji cha mchezaji

Kufundisha Wanaume na Wanawake ndani ya msimu mmoja na wote wakapata mafanikio sio jambo jepesi na sio kila Kocha anaweza ni Juma Mgunda pekee

Inaweza kuja hoja ya Ubingwa lakini haina mashiko, Kuna Mbwana Makata alikua kuwa bora kwa sababu ya kuinusuru Kagera Sugar kushuka daraja, Mecky Mexime aliwahi Kocha bora kwa kuzalisha kuendeleza vipaji na kuitengeneza Mtibwa Sugar kuwa timu tishio kama anavyofanya Mgunda hivi sasa

Sababu ya mwisho kwanini Juma Mgunda ndio Kocha bora ni nidhamu na heshima aliyonayo

Kocha Mgunda hajawaji kutukana Mwamuzi, hajawahi kupigana na wala hajawahi kuingia Uwanjan kufanya vurugu" Ahmedy Ally

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad