Akamatwa Akiwa na Milioni 29 za Wizi Gesti

 

Akamatwa Akiwa na Milioni 29 za Wizi Gesti

Mkazi wa Jijini Dar es salaam amekamatwa na Polisi Mkoani Njombe akiwa na Tsh. 29,374,000 katika nyumba ya kulala Wageni (Gesti) Mjini Makambako ambapo fedha hiyo inadaiwa ameipata kwa njia ya wizi.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga, amesema wamemkamata Mwakatundu wakiwa wanafanya upekuzi wa kawaida katika nyumba za kulala Wageni ambapo baada ya mahojiano amekiri kuipata fedha hiyo kwa njia ya uporaji.


“Tulipofika katika nyumba ya kulala Wageni ambayo inaitwa Lisbon ndio tulifanikiwa kumkamata akiwa na fedha hiyo lakini baada ya kumuhoji kwa kina alieleza kwamba fedha hizo amezipora katika kampuni aliyokuwa anafanyia kazi ya Interchick Dar es Salaam”


Amesema tayari Mtuhumiwa amekwishakabidhiwa kwa Jeshi la Polisi Mkoani Dar es salaam kwa ajili ya hatua nyingine za kimashtaka ili aweze kufikishwa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad