Timu ya Al Ahly imefanikiwa kutwaa tena taji la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Espérance Sportive de Tunis katika mchezo wa marudiano wa Fanali usiku wa jana Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo nchini Misri.
Bao pekee la Al Ahly amejifunga kiungo Mtogo, Roger Ben Boris Aholou dakika ya nne akijaribu kuokoa. Ikumbukwe mechi ya kwanza timu hizo kutoa sare ya bila mabao Mei 18 Uwanja wa Olympique Hammadi Agrebi Jijini Radès nchini Tunisia.
Kwa kutwaa taji hilo la 12 la Ligi ya Mabingwa, Al Ahly watazawadiwa dola za Kimarekani Milioni 4, wakati Esperance watapata dola Milion