Ali Kamwe Awapiga Dongo SIMBA 'Kombe la Shirikisho ni Kombe la Loser na Ma Loser'
Ofisa Habari wa Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa mara ya tatu mfululizo, Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amewapiga dongo watani zao Simba SC kwa kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu huku wakiangukia Kombe la Shirikisho Afrika badala ya Ligi ya mabingwa ambayo wamekuwa wakifanya vizuri kwa misimu kadhaa.
Kamwe amesema hayo baada ya kumalizika kwa ligi hiyo huku wakifanikiwa kumalizka nafasi ya kwanza wakiwa na alama 80 na kupata tuzo ya mfungaji bora ambaye ni Aziz KI aliyefunga mabao matatu katika mchezo wa leo dhidi ya Tanzania Prisons.
“Furaha yetu imekamilika leo baada ya Simba kuelekea rasmi Kombe la Shirikisho. Sasa tunawashauri waanze kutafuta hoteli Djibout, Ethiopia, Eritrea, Shelisheli, Somalia, Sudan Kusini waangalie huko hoteli gani nzuri kwao. Unaweza kupangiwa sehemu ukakutana na hoteli kuna mbu wengi kweli.
“Sisi tulipitia mazito mpaka kufikia fainali lakini tulivumilia tu, Simba wanakwenda kukutana na mbu wanaweza kwenda huko wazima wakarudi na mbu.
“Sisi wa Kimataifa na wenzetu Azam ni Misri, Morocco, Congo Dr, yani Congo huwezi kwenda kama unacheza Shirikisho. Niwambie shirikisho ni Kombe dogo, ni kombe la loser na ma-loser wamekwenda huko, watu wasiojua wameenda huko, tutumie maneno yaleyale msibadilishe maneno.
“Kile kichaka cha was aba fyuuu! Shirikisho ili uongeze pointi lazima ujikaze kama Yanga uende fainali. Msimu ujao tukiingia makundi kile kichaka tunakifyeka na ile nafasi ya saba tunakaa sisi pale. Yanga tulikuwa tunamsubiri Eng. Hersi atulete hapa," amesema Kamwe