Bondia Oleksandr Usyk wa Ukraine usiku wa jana amemshinda Muingereza Tyson Fury kwa pointi za majaji kupishana, 2-1 ukumbi wa Kingdom Arena Jijini Riyadh, Saudi Arabia na kuwa bingwa wa kwanza asiyepingika wa uzito wa juu wa mataji manne.
Jaji mmoja tu alimpa ushindi Fury wa pointi 114-113, wakati wengine wawili walimpa Usyk ushindi wa pointi 115-112 na 114-113, hivyo kuwa bingwa mpya asiyepingika duniani uzito wa juu akihodhi mataji ya WBC, WBA, IBF na WBO.
Lilikuwa pambano la aina yake, Fury akianza kutawaka raundi za mwanzo, kabla ya Usyk kuzinduka baadaye na kufanikiwa hadi kumpeleka chini Gypsy King raundi ya tisa.
Hata Hivyo, baada ya pambano hilo Fury alidai watu wanaegemea upande wa Usyk kwa sababu vita inayoendelea nchini kwao, Ukraine.