Mkali wa muziki wa amapiano, Issaya Mtambo 'Chino Kidd' ambaye sasa anafanya vizuri na wimbo wa Binadamu amesema licha ya changamoto ya ushindani kwenye sanaa amejipata anaweza kufanya kila kitu kulingana na fedha anazoingiza.
Chino Kidd alianza kuwa mnenguaji kwenye kazi za Omary Mwanga 'Marioo' sasa ameingia kwenye sanaa ya kuimba na kuonesha ushindani mkubwa kwa wakubwa walio mtangulia kwenye sanaa hiyo hadi kufikia kazi zake kushindanishwa na #Diamond.
Akizungumza na Mwananchi amesema sanaa imeanza kumpa matunda anafurahia na kujiona alikuwa anachelewa kuingia huko kutokana na sasa kuanza kumiliki baadhi ya vitu vya ndoto yao.
"Muziki umenilipa ila bado naendelea kuutumikia kwa ajili ya kufikia malengo yangu najivunia hilo kwani nimejipata nimeweza kumiliki magari ya ndoto yangu, naishi vizuri na sasa matamasha yamekuwa mengi," amesema na kuongeza;
"Mbali na sanaa hii kunifikisha sehemu nzuri ndoto yangu ya kuwa na kituo cha vijana wanenguaji ipo pale pale kwani nimetoka huko hadi hapa nilipo njia yangu ni kunengua lazima niwapitishe wengine watakuwa na mabadiliko yao." amesema.