Clatous Chama wa Simba Afungiwa na Kupigwa Fine na Bodi ya Ligi

Clatous Chama wa Simba Afungiwa na Kupigwa Fine na Bodi ya Ligi


MICHEZO: KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Aprili 30, 2024 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatayo;

Mchezaji Clatous Chama wa klabu ya Simba amefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh. 1,000,000 kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi mchezaji Nickson Kibabage wa klabu ya Yanga wakati mchezo tajwa hapo juu ukiendelea.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 41:5(5.2) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad