Dereva wa pikipiki ya Afisa mifugo Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, Abel Adamson Mwaipopo (25) amefariki Dunia baada kumgonga ndege aina ya bundi na kisha pikipiki yake kupoteza mwelekeo na kuanguka na hatimaye kupoteza maisha yake.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Albert Msando amesema tukio hilo limetokea mapema leo katika eneo la Sindeni jirani na kona ya PRS ambapo Dereva huyo alikuwa akiendesha pikipiki yenye namba za usajili STM 0232 .
Msando amesema “Kwanza naomba nitolee ufafanuzi jambo hili kwani aliyefariki sio Afusa mifugo kama wengi walivyosema kwani Afisa mifugo wetu wa Wilaya ni Mwanamke na aliyefariki ni Mwanaume Dereva ambaye anamwendesha Afisa mifugo”
“Ajali ni kama ajali nyingime lakini akishahusishwa bundi mara zote tayari kunakuwa na hizo imani za kishirikina na hofu kwa Watu kwamba amegonga bundi kafa na yeye mwenye amekufa lakini vilele inawezekana kwa kiasi kikubwa labda alivyomuona bundi katika kujaribu kumkwepa hakuchukua tahadhari akapata ajali ni uwezekano vilevile hakuwa amevaa kofia ngumu hivyo katika kuanguka akajigonga akapata madhara akafariki hivyo inawezekana ikawa ni ajali ya kawaida lakini kwasababu imemuhusisha bundi lazima ita letataharuki kuwa inahusiana na mambo ya kishirikina”
Msando amesema kama Serikali ngazi ya Wilaya wana amini ni ajali kama ajali nyingine zinazotokea barabarani na hivyo ametoa wito kwa wale wote wanao tumia vyombo vya moto hususa pikipiki kuvaa kofia ngumu na kuchukua tadhari pindi wanapo kuwa barabarani na kutokwenda kwa spidi ili kuweza kuepuka kupata ajali.