Dortmund kubeba pesa nyingi wakifungwa Madrid kuliko wakibeba UEFA

 

Dortmund kubeba pesa nyingi wakifungwa Madrid kuliko wakibeba UEFA

Unaambiwa klabu ya Borussia Dortmund itanufaika zaidi endapo itashindwa kutwaa kombe la UEFA mbele ya Real Madrid kuliko ambavyo ingeshinda kombe hilo. Yaani kwa lugha rahisi ni kwamba Dortmund itapata pesa nyingi kama ikifungwa kuliko kama ingeshinda yenyewe.


Endapo Borussia Dortmund itashinda fainali hiyo ya UEFA mbele ya Madrid watalipwa kitita cha pauni milioni 20 (Tsh bilioni 52.75) kama zawadi ya mshindi wa kombe hilo.


Lakini kama Dortmund ikifungwa na kisha Madrid kutwaa ubingwa wa kombe hilo la UEFA basi Real Madrid watailipa Borussia Dortmund kitita cha pauni milioni 25 (Tsh bilioni 64.69) kama malipo ya bonasi kwenye mkataba wa mauzo ya kiungo Jude Bellingham kutoka Dortmund kwenda Real Madrid.


Je, ingekuwa wewe ni Dortmund ungechagua nini, ushinde kombe upate Mil 20 au ufungwe upate Milioni 25?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad