Fei Toto Awakataa Mashabiki wa SOKA...."Sishindani na Mtu Uwanjani"

 

Fei Toto Awakataa Mashabiki wa SOKA...."Sishindani na Mtu Uwanjani"

Kiungo kutoka visiwani Zanzibar na Klabu ya Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema kila anachokifanya uwanjani ni kwa ajili ya timu yake na anapofunga hakuna anayeshindana naye, bali ni kuipa matokeo mazuri timu yake.

Nyota huyo amesema anafurahi kuona anaisaidia zaidi timu yake kuweza kupata matokeo mazuri katika kila mchezo.

Azam FC leo Alhamis (Mei 09) imeshuka uwanjani kuumana na Simba SC kwenye mfululizo wa michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayokwenda ukingoni.

“Kila ninachokifanya uwanjani ni kwa ajili ya timu yangu, sichezi kwa kushindana na mtu, nacheza kuisaidia timu kufanya vizuri, nashukuru Mungu kwa kila kitu kizuri ninachokifanya kwa ajili ya timu, ushindi tunaopata niwe nimefunga mimi au mtu mwingine unatokana na jitihada na juhudi za wachezaji wote,” amesema Fei Toto.

Fei Toto mpaka sasa ameifungia timu yake mabao 15 na kutoa pasi za magoli ‘asisit’ saba akilingana na kiungo wa Young Africans, Azizi Kii.

Mashabiki wa soka nchini tayari wameanza kuwashindanisha nyota hao kutokana na kasi yao ya kufunga huku wakiwa wamelingana idadi ya mabao ya kufunga na wanaamini mfungaji bora msimu huu atatoka kati yao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad