Huduma za Vivuko Kusimamishwa Kupisha Kimbunga Hidaya

 

Huduma za Vivuko Kusimamishwa Kupisha Kimbunga Hidaya

Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) umetoa taarifa kwa Watumiaji wa vivuko katika baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia, Mkoa wa Dar es salaam pamoja na Tanga kwamba, kutakuwa na kusimama kwa utoaji wa huduma ya vivuko katika maeneo hayo ili kujilinda na kuepukana na athari zozote ambazo zinaweza kujitokeza kutokana na kimbunga HIDAYA na kusababisha athari kwa Watumiaji wa vivuko.


TEMESA imesema inaendelea kufuatilia taarifa za Hali ya Hewa zinazoendelea kutolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini ili kuhakikisha abiria wote wanaotumia huduma hizo wanakuwa salama wakati wote.


“TEMESA pia inaendelea kuwaomba radhi abiria wote kutokana na changamoto husika inayosababishwa na uwepo wa kimbunga hicho na inawakumbusha kuendelea kufuata maelekezo ya Mabaharia wakati wote wanapotumia vivuko ili kuendelea kuwa salama”


TEMESA imesema jana May 03,2024 vivuko vilisimama kufanya kazi baada ya upepo kuwa mkali baharini na leo na siku zijazo vitaendelea kusimama hadi pale Mamlaka za Hali ya Hewa zikitoa taarifa nyingine.


Moja ya vivuko viliyosimamisha huduma ni MV. kilindoni ambacho kilitakiwa kutoka Mafia kwenda Nyamisati saa saba usiku wa kuamkia leo lakini hakikutoka kwasababu ya upepo mkali na hivyo kusubiri hadi hali ya bahari ikiwa nzuri na Mamlaka kutangaza vinginevyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad