John Bocco Awaanga SIMBA Rasmi, Aandika Haya




Baada ya kudumu misimu saba ndani ya Simba, nahodha wa timu hiyo, John Bocco amewaaga mashabiki na mastaa wenzake wa timu hiyo kwa kuweka wazi kuwa huu ndiyo mwisho wake wa kuonekana ndani ya kikosi hicho akicheza.

Bocco kupitia mtandao wake wa kijamii ameandika: "First and Last thanks Lion" akiwa na maana kwamba ni mwanzo na mwisho, asanteni Simba na kuwaibua mastaa mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali ambao wamemtakia kila la heri katika maisha yake mapya.

Akichangia katika maneno hayo ya Bocco, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA amendika: “Umefanya kazi yako kwa usahihi na kwa uaminifu muda wote, mfano mzuri sana asante.”

Mbunge wa Jimbo la Nzega na shabiki kindakindaki wa Simba, Dk Khamis Kigwangala ameandika: “Tukijenga jengo la maana wewe ni miongoni mwa wachezaji ambao jina lako linapaswa kuandikwa kwa wino wa dhahabu ama kujengewa sanamu. Wewe ni Simba kweli.”

Naye kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama ameandika: “Nahodha asante sana, heshima kwako.”; ilhali kiungo mkabaji wa Ghazl El Mahalla ya Misri na Taifa Stars, Himid Mao akisema: “Hongera mwanangu Mhaya wa kwanza kuwa mchezaji.”

Kwa upande wake, mshambuliaji wa PAOK ya Ugiriki na nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amemtakia heri Bocco akisema: “Hongera na kila lakheri katika ukurasa wako mpya.”

Bocco alijiunga na Simba katika msimu wa 2017/18, hivyo ameitumikia timu hiyo kwa misimu saba akitwaa mataji ya ligi na michuano mbalimbali, huku akiisaidia timu hiyo kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara tano.

Mchezaji huyo amewaaga wana Simba baada ya mkataba wake na timu hiyo kumalizika na alikuwa nje ya timu kwa muda mrefu akijiuguza majeraha huku akiinoa timu ya vijana Simba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad