Kibu, Fred Waondolewa Kikosini Simba, Chama Arejeshwa

Kibu, Fred Waondolewa Kikosini Simba, Chama Arejeshwa


Klabu ya Simba imesema kuwa kuelekea mchezo wao wa leo wa Ligi Kuu dhidi ya Dodoma Jiji itawakosa nyota wake wawili ambao ni Kibu Denis na Fred Michael kutokana na majeruhi yanayowasibu.


Hayo yamesemwa jana na Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally wakati akizungumzia hali ya kikosi chao kuelekea mchezo huo utakaopigwa leo katika dimba la Azam Complex, Chamazi Dar es Salaam.


“Kitu cha kufurahisha zaidi ni kurejea kwa nyota wetu kadhaa waliokuwa majeruhi, Saido Ntibazonkiza, Mwamba wa Lusaka Clatous Chama ambaye naye amekosekana kwenye michezo kadhaa nyuma tangu tutoke Zanzibar amekosa michezo kama mitatu, kama Mungu akijalia kesho (leo) atarejea dimbani kuipigania tena Simba yake na Jose Luis Miquissone. Hii ni faraja kwetu.


“Kibu Denis tutaendelea kumkosa, anaendelea na matibabu hata mazoezini bado hajarudi, anapatiwa matibabu huko huko mpaka atakapofanyiwa vipimo tena ndipo madaktari watatuambia ni muda gani atakuwa tayari kurejea dimbani kuitumikia Simba.


“Fredy Michael yeye alishindwa kuendelea na mchezo dhidi ya Dodoma Jiji kipindi cha pili akafanyiwa mabadiliko. Baada ya kutoka Dodoma ameendelea na matibabu na ahajafanya mazoezi na timu kwa siku mbili na leo (jana) hakuwa sehemu ya wachezaji ambao wamefanya mazoezi, maana yake ni kwamba ataukosa mchezo wa kesho (leo). Baada ya mchezo huo atafanya vipimo na watatuambia atakosekana kwenye michezo mingapi.


“Ayoub Lakred alikosekana mchezo dhidi ya Dodoma, alikuwa akisumbuliwa na mgongo lakini sasa hivi yuko sawa amesharejea kwenye mazoezi na leo ni katika sehemu ya wachezaji ambao wamefanya mazoezi na atakuwa sehemu ya kikosi kesho dhidi ya Geita Gold. Kwa hiyo tutawakosa wachezaji wawili tu ambao ni Kibu na Fredy lakini wengine wote wapo tayari kuipambania Simba yao,” amesema Ahmed Ally.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad