Kimbunga "IALY" kinazidi kusogea Pwani ya bahari

 

Kimbunga "IALY" kinazidi kusogea Pwani ya bahari

Taarifa kutoka mamlaka ya Hali ya hewa Nchini (TMA) kuhusu mwenendo wa kimbunga IALY zimeonyesha kimbunga hicho kinazidi kusogea maeno ya pwani ya bahari ya Hindi 


Akizungumza na EATV mchambuzi wa masuala ya hali ya hewa kutoka TMA Rose Senyagwa amesema huenda kimbunga hicho hadi kufikia majira ya usiku kikawa kimekaribia maeneo ya Pwani ikiwemo mikoa ya Dar es salaam, Pwani Lindi na Mtwara ambapo amesema taarifa zaidi zitaemdelea kutolewa kadri muda unavyokwenda 


Amesema miongoni mwa kundi linalopaswa kuchukua tahadhari ni wavuvi na wote wanaopenda kutembelea maeneo ya fukwe wanapaswa kuichukua tahadhari dhidi ya uwepo wa kimbunga hicho 


Mwisho amewasisitiza wananchi kutodharau au kubeza taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya hali ya hewa kwasababu kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Kimataifa la utabiri wa hali ya hewa zinaonyesha taarifa za utabiri zinazotolewa Nchini Tanzania ni za uhakika kwa zaidi ya asilimia 90

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad