KIMENUKA..Watumishi 7 Arusha Wahojiwa TAKUKURU

 

KIMENUKA..Watumishi 7 Arusha Wahojiwa TAKUKURU

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Arusha, imesema imewahoji watumishi saba wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, kufuatia tuhuma za kughushi nyaraka, uchepushaji wa makusanyo ya Serikali na ubadhirifu wa fedha za umma.


Akizungumza leo Jumatano Mei 22, 2024, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Arusha, Zawadi Ngailo amesema miongoni mwa watumishi ni wa kitengo kinachohusiana na ukusanyaji wa mapato.


“Tunaendelea kuwahoji na wengine pia, tunakusanya nyaraka kwa ajili ya kutambua nini kimetokea na watakaothibitika kushiriki watafikishwa mahakamani,” amesema Ngailo.


Amesema bado wataendelea kuwahoji watumishi wengine sambamba na kuperuzi nyaraka mbalimbali kwa lengo la kubaini kilichotokea na wataangalia kwenye mfumo. “Kwa sababu suala hili linahusu matumizi ya mfumo, tukikamilisha uchunguzi tutatoa taarifa,” amesema ofisa huyo.


Suala la ubadhirifu liliibuliwa mwishoni mwa wiki katika kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda na wadau wa utalii katika kikao kilicholenga kusikiliza na kutatua changamoto zilizoko katika sekta hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad