Kisa Cha Sarah Kuachana na Diamond Hichi Hapa, Wema Sepetu Kahusika


Kisa Cha Sarah Kuachana na Diamond Hichi Hapa, Wema Sepetu Kahusika

Sarah, mrembo wa KAMWAMBIE aliyekuwa mpenzi wa Diamond Platnumz, amesimulia kisa cha kuachana mazima na msanii huyo wa Bongo Fleva kwenye interview na Wasafi FM, siku chache baada ya kurudisha mahusiano yao yaliyodumu kuanzi mwaka 2007 hadi 2009, kabla ya kuvunjika.

Mwaka 2010, baada ya Diamond kuachia albamu yake ya kwanza, KAMWAMBIE, na kupata mafanikio makubwa, alipata fursa ya kufanya maonyesho Ulaya. Wakati huo, alimtafuta Sarah na kumwomba warudiane ili amuoe.

"Baada ya kutoa albamu ya kwanza, Kamwambie alipata mafanikio makubwa hadi kununua gari na kwenda kupanga nyumba. Wakati huo, naishi Kinondoni, nishakuwa na maisha yangu. Alinitafuta na tukaenda Coco Beach, wakati huo wamoto, anahela, anaomba turudiane ili anioe", alisema Sarah.

Sarah alidai ombi lake lilijibiwa siku kadhaa baadae baada ya kutafakari kutokana na historia yao ya zamani. Baada ya hapo, Diamond alimwambia kuwa anasafiri kwenda Ulaya lakini ajiandae kwa kila kitu atakaporudi Bongo wataenda kuishi pamoja.

"Nasafiri naenda Ulaya kwa Show, nikirudi naomba ukusanye kila kitu chako twende tukakae pamoja. Tukawa tuko vizuri kabisa", aliongeza Sarah.

Hata hivyo, baada ya siku kadhaa kupita, Sarah alienda kwenye Show Bilicanas akiwa chooni aliingia Wema Sepetu akiwa ametoka Ulaya kisha akaingia VJ Penny na kukumbatiana kwa furaha huku Wema akimwambia twende ukamuone shemeji yako.

[Penny] "Twende nikamuone shemeji yangu aliyekurudisha Tanzania, maana uliniambia hutaki kurudi tena huku”, ambapo Sarah ameongeza kuwa wakati “Wanaondoka mimi nikawafuata nyuma, Wema alikuwa maarufu na mimi nikasema ngoja nimuone huyo boyfriend wake, nafika counter ya chini boyfriend mwenye ni Naseeb, nikiwa nimesimama juu, Wema anaenda kumtambulisha Penny kwa Naseeb".

Hii ilimfanya ajisikie vibaya kutokana na ahadi ya Diamond ya kuishi naye, licha ya kujua kuwa alikuwa na mwanamke mwingine lakini pia kurudi Bongo bila ya kumtaarifu chochote.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad