Kocha Gamondi Awamwagia Sifa Nyota wake

 

Kocha Gamondi Awamwagia Sifa Nyota wake

Kocha Mkuu wa Young Africans SC, Miguel Gamondi, amesema kutokana na aina ya wachezaji alionao kikosini inampa nafasi ya kumtumia yeyote na kupata matokeo chanya.


Gamondi ameyasema hayo baada ya kushuhudiwa mchezo uliopita dhidi ya Dodoma Jiji kubadili kikosi kwa kiasi kikubwa na kupata ushindi mnono wa magoli 4-0.


Katika mchezo huo, wachezaji wengi waliotumika hawakuwa wakipata muda mwingi sana wa kucheza msimu huu lakini walichangia kwa kiasi kikubwa kupata ushindi huo mnono.


“Mimi nawaamini wachezaji wangu ndio maana nafanya mabadiliko ya mara kwa mara. Najaribu kuwapa nafasi wengine kufanya kile walicho nacho kwa sababu wote wananipa kila ninachokitaka kwenye uwanja wa mazoezi,” alisema Gamondi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad