Kocha Juma Mgundu Afunguka: Haijaisha Mpaka iishe

 

Kocha Juma Mgundu Afunguka: Haijaisha Mpaka iishe

Kaimu Kocha Mkuu Simba SC, Juma Mgunda amesema kuwa malengo yake ni kuhakikisha anashinda michezo yote mitatu iliyosalia ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kumaliza wa pili kwenye msimamo wa ligi.


Mgunda amesema hayo baada ya Simba kupata sare mbele ya Kagera Sugar na kufanya walingane kwenye alama na Azam iwapo wote watashinda michezo yao iliyosalia huku Azam akiwa na faida ya idadi kubwa ya tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.


"Bado hatujamaliza michezo yote, tulipambana kwenye mchezo dhidi ya Kagera lakini bahati haikuwa kwetu, tunajipanga kwa ajili ya mchezo ujao, kwangu mimi bado haijaisha, bado tuna nafasi ya kumaliza kwenye nafasi ya pili, kikubwa tunatakiwa kufanyia kazi mapungufu tuliyaona ili michezo iliyobaki tupate alama tatu.


“Tutaendelea kupambana, nimewaambia wachezaji wangu wasikate tamaa, waendelee kupambana na kuweka mkazo kwenye michezo yote iliyobakia, hatutaki kuangalia matokea ya timu nyingine, tupambane sisi kushinda michezo yote, naamini tunaweza kufanya vizuri kwenye mechi zote zilizobakia,” amesema Mgunda.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad