LHRC Yamuonya RC PAUL Makonda Kwa Kumdhalilisha Mtumishi wa Longido



LHRC Yamuonya RC PAUL Makonda Kwa Kumdhalilisha Mtumishi wa Longido


Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa taarifa ya Onyo kwa Mkuu wa Mkoa Arusha, Paul Makonda baada ya kuonekana kwenye Video akitoa kauli za udhalilishaji dhidi Mtumishi wa Kike kutoka Longido


“Tumepokea kwa masikito Video inayomuonesha Mkuu wa Mkoa wa Arusha akimdhalilisha Mtumishi wa jinsia ya Kike kule Longido. Tunakemea vikali kauli hizo hasa kwa Mtu kama yeye (Mkuu wa Mkoa)”


Aidha, LHRC imemtaka Makonda kuomba radhi na kuacha tabia hiyo kwasababu inatweza Utu wa Mwanamke na kushusha juhudi za kutetea Haki za Wanawake huku ikielezwa kuwa Viongozi kama yeye wakitoa kauli zinatoa mifano mibaya kwa watu wengine


Kupitia Video hiyo, RC Makonda anasikika akimtaka Mtumishi huyo kuzungumza vizuri na si kama “anaongea na mtu anayetaka kumposa au yuko kwenye Kitchen Party na pia yeye (RC) ana Mke mzuri”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad