Mama Amteka Mwanae wa Kumzaa ili Mumewe Atoa Shilingi Milioni 20




Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limesema linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kumteka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitano, mwanafunzi wa shule ya Awali ya Isaiah Samartan jijini humo ambaye aliripotiwa kupotea Mei 15, mwaka huu.

Akitoa taarifa hiyo Msemaji wa Jeshi la Polisi Naibu Kamishna wa Polisi, David Misime amesema tukio hilo liliripotiwa na baba mzazi wa mtoto Layson Mkongwi, mfakanyakazi wa Kampuni binafsi ambaye alipokea simu kutoka kwa mtu asiyefahamika na kumweleza kuwa hatampata mtoto wake hadi atakapomtumia kiasi cha shilingi milioni 20.

Misime amesema baada ya kupokea taarifa hizo Jeshi lilianza uchunguzi na kufanikiwa kumpata mtoto akiwa salama pamoja na mtuhumiwa, Winfred Martin Komba (36) ambaye ndiye aliyekuwa akimpigia simu baba wa mtoto huku mtuhumiwa mwingine akiwa ni mama mzazi wa mtoto huyo, Agnes Mwalubuli ambaye alipanga njama ili kujipatia fedha hizo kutoka kwa baba wa mtoto huyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad