Matokeo Al Ahly na Esperance Nusu Fainali ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika

Matokeo Al Ahly na Esperance Nusu Fainali ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika



TUNIS, TUNISIA: NGOMA droo. Ndicho kilichotokea kwenye mchezo wa kwanza fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya Esperance de Tunis kutoka sare ya bila kufungana na Al Ahly katika kipute kilichofanyika usiku wa Jumamosi.

Katika mchezo huo, mashuti 20 yalipigwa, 10 kwa kila upande, lakini ni shuti moja tu lililolenga goli, kwa upande wa wababe wa Misri, Al Ahly.

ES Tunis ikiwa nyumbani, ilishindwa kuonyesha makali yaliyotarajiwa, ikishindwa kupata kona hata moja, huku wapinzani wao, wakipiga kona tatu katika mchezo huo.

ES Tunis ilizuia mashuti mawili katika mchezo huo, ambao ilimiliki mpira kwa asilimia 53, wakati Ahly iliyomiliki mpira kwa asilimia 47, yenyewe ilizuia mashuti manne.

Pasi 444 zilipigwa na wenyeji ES Tunis, wakati Al Ahly ilipiga pasi 397, huku sehemu kubwa ya mchezo huo ikipigwa kwenye eneo la kati la uwanja.

Mechi ya marudiano itafanyika wiki ijayo, huko Misri, huku matokeo hayo ya mechi ya kwanza yakiipa faida ES Tunis, kwani sare yoyote ya mabao katika mechi hiyo ya ugenini itawafanya kunyakua ubingwa. Itakuwaje? Ngoja tuone.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad