Mbwana Samatta, Novatus Dismas Katika Rekodi za Kipekee za Kutwaa Ubingwa Ulaya

 

Mbwana Samatta, Novatus Dismas Katika Rekodi za Kipekee za Kutwaa Ubingwa Ulaya



Mwezi Mei umekuwa wa kihistoria kubwa kwa nyota wawili wa Kitanzania wanaocheza soka la kulipwa katika klabu tofauti barani Ulaya, Mbwana Samatta na Novatus Dismas baada ya timu zao kufanikiwa kutwaa mataji ya Ligi Kuu katika nchi zilipo.


Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mbwana SamattaMbwana Samatta alifanikiwa kuvaa medali ya ubingwa wa Ligi Kuu ya Ugiriki baada ya timu yake PAOK kumaliza ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ikikusanya pointi 80.


Ingawa Samatta hakupata muda wa kutosha wa kucheza katika kikosi cha PAOK, ameshiriki katika mafanikio hayo kwa kufunga mabao mawili kati ya 87 ambayo timu hiyo imepachika msimu huu katika mbio za kusaka ubingwa huo.


Hilo Hilo ni taji la pili la Ligi Kuu kwa Samatta kulitwaa barani Ulaya ambapo la kwanza alichukua katika msimu wa 2018/2019.


Wakati Samatta akifanya hivyo huko Ugiriki, nyota mwingine wa Taifa Stars, Novatus Dismas amefanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu ya Ukraine akiwa na timu ya Shakhtar Donetsk ambalo ni la kwanza kwake la Ligi Kuu barani humo.


Kabla ya hapo, Dismas alicheza katika ligi mbili tofauti barani Ulaya bila kuvaa medali ya ubingwa ambapo kwanza ilikuwa ni Ligi Kuu ya Israel katika timu ya Maccabi Tel Aviv na kisha ligi ya Ubelgiji katika timu ya Zulte Waregem.


Kitendo cha timu za nyota hao wawili kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwenye nchi zao kinawafanya waingie katika orodha ya wachezaji wa Kiafrika ambao wamemaliza msimu vizuri kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na mashindano mbalimbali tofauti ambayo zimeshiriki barani Ulaya huku wengi wakichangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa mafanikio hayo.


Spoti Mikiki inakuletea orodha ya ligi na mashindano tofauti msimu huu wa 2024/2025 ambayo yamemalizika vyema kwa nyota wa Kiafrika wakifanikiwa kuvaa medali za ubingwa kwenye shingo zao huko Ulaya na maeneo mengine duniani;


Europa League Nyota wa Nigeria, Ademola Lookman amemaliza vyema msimu wa 2023/2024 baada ya kuiongoza Atalanta kutwaa ubingwa wa mashindano ya Europa League ambayo yanashika nafasi ya pili kwa thamani kwa ngazi ya klabu barani humo.


Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, alifunga mabao yote katika ushindi wa mabao 3-0 ambao Atalanta ilupata dhidi ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani katika mechi hiyo ya fainali iliyochezwa katika Uwanja wa Aviva huku Dublin, Ireland.


Mbali na Lookman, Mwafrika mwingine aliyevaa medali katika kikosi cha Atalanta katika mechi hiyo iliyochezwa Jumatano iliyopita ni mshambuliaji wa Mali, El Blali Toure.


Hata kama Lookman na Toure wasingechukua ubingwa katika mechi hiyo, bado bendera ya Afrika ingepeperushwa kutokana na uwepo wa wachezaji watano kutoka barani humu kwenye kikosi cha Leverkusen ambao ni Edmond Tapsoba (Burkina Faso), Amine Adli (Morocco), Victor Boniface na Nathan Tella (Nigeria) pamoja na Odilon Kossounou wa Ivory Coast.


Ligi Kuu Hispania 'La Liga'


Pazia la Ligi Kuu ya Hispania 'La Liga' msimu huu lilifungwa rasmi Jumamosi iliyoppita huku Real Madrid ikifanikiwa kutwaa ubingwa, Barcelona ikimaliza katika nafasi ya pili na Girona ikiangua nafasi ya tatu.


Hakuna namna unayoweza kumtenganisha kiungo wa Morocco, Brahim Diaz na taji hilo kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwa kuitumikia timu hiyo kwa zaidi ya dakika 1550 huku akifunga mabao nane kabla ya mechi ya mwisho ya kufungia msimu ambayo ilicheza na Real Betis.


Diaz anayo nafasi nyingine ya kuipeperusha bendera ya Afrika katika Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa Real Madrid  itaibuka na ushindi katika mechi ya fainali dhidi ya Borussia Dortmund itakayochezwa, Juni Mosi.


Ligi Kuu Ujerumani 'Bundesliga' Nyota watano wa Afrika walimaliza vizuri msimu wa Ligi Kuu ya Ujerumani kwa kutwaa ubingwa wakiwa na kikosi cha Bayer Leverkusen ambacho kilimaliza msimu bila kupoteza mechi hata moja ya ligi.


Edmond Tapsoba (Burkina Faso), Amine Adli (Morocco), Victor Boniface na Nathan Tella (Nigeria) pamoja na Odilon Kossounou wa Ivory Coast ni wachezaji hao ambao hawajamaliza kinyonge msimu wa Bundesliga.


Ligi Kuu Ufaransa 'Ligue 1' PSG ilimaliza kibabe msimu wa Ligi Kuu Ufaransa 2024/2025 kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu nchini humo ambao ulikuwa wa tatu mfululizo kwao.


Katika kikosi cha PSG kilichoondoka na taji hilo msimu huu, yumo beki wa Morocco, Achraf Hakimi ambaye licha ya kucheza nafasi ya ulinzi, amefunga mabao manne ya timu hiyo kwenye Ligue 1 katika msimu uliomalizika.


Ligi Kuu Saudi Arabia Msimu ulimalizika vyema kwa mastaa wawili wa Afrika wanaoitumikia Al Hilal inayoshiriki Ligi Kuu ya Saudi Arabia, kipa Yassine Bounou na beki Kalidou Koulibaly baada ya kufanikiwa kutwaa taji la ligi kuu nchini humu msimu huu.


Bounou mwenye umri wa miaka 31, amecheza mechi 31 msimu huu na leo inaweza kuwa ya 32 wakati timu yake itakapokabiliana na Al Wehda kati ya michezo 34 ya ligi hiyo. Kwa upande wa Koulibaly wa Senegal mwenye umri wa miaka 32, amecheza mechi 29 za timu hiyo msimu huu kwenye Ligi Kuu ya Saudi Arabia.


Ligi Kuu Ureno Nyota wawili wa Kiafrika wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Ureno wakiwa na Sporting Lisbon ambayo hilo ni taji lake la 20 la ligi hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka 1906.


Wachezaji hao ni beki wa Ivory Coast, Ousmane Diomande na mshambuliaji wa Msumbiji, Geny Catamo.


Kwingineko Kiungo wa Morocco, Ismael Saibari amefanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu Uholanzi akiwa na kikosi cha PSV Eindhoven.


Huko Serbia, Nasser Djiga (Burkina Faso), Guelor Kanga (Gabon), Peter Olayinka (Nigeria), Othman Bukari (Ghana), Pape Ndiaye (Senegal) na Jean Krasso (Ivory Coast) walitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya huko wakiwa na Red Star Belgrade

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad