Mchambuzi: Simba Kumaliza Nafasi ya PILI Wasahau Kabisaaaa

 

Mchambuzi: Simba Kumaliza Nafasi ya PILI Wasahau Kabisaaaa

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka Clouds Media, Master Tindwa amesema kwa mwenendo ulivyo ni kama Ligi imeisha na uwezekano wa Simba kumaliza nafasi ya pili ni mdogo sana.

Simba ambaye analingana na Azam kwa alama 63 kila mmoja lakini Azam yupo juu kwenye msimamo wa ligi kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa huku kila mmoja akipigania nafasi ya pili ili aweze kushiriki Klabu Bingwa Afrika msimu ujao.

“Kama Azam atafunga goli moja kila mechi kwa mechi zilizobaki, Simba inabidi wafunge magoli manne kila mechi ili wamalize nafasi ya pili, inawezekana lakini sio rahisi.

“Naona nafasi ya pili kwa Simba ni ngumu , Ligi tayari imeisha wa mwisho watakuwa walivyo na juu itabaki ilivyo ,Kila mtu anaomba ashinde mechi zake na mwisho wa siku Azam tayari anafaida,” amesema Tindwa.

Mechi za Simba zilizobaki

Vs KMC

Vs JKT Tanzania

Mechi za Azam zilizobaki

Vs Kagera

Vs Geita.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad