Muigizaji maarufu nchini Uingereza,Brian Deacon,ambaye alicheza filamu ya Yesu (Story of Jeasus Christ) iliyoanza kurekodiwa mnamo mwaka 1977 na kumalzika mwaka 1979,ameigongelea msumari kauli yake ya kwamba kila mtu amuabudu Mungu, wake aliye rohoni, na amtafute Mungu wa kweli, kwani yeye alikuwa ni muigizaji tu na alipomaliza kucheza filamu hiyo, alilipwa chake na kusepa,lakini anashangaa picha yake hiyo iko kila kona huku watu wengine wameweka ndani kwenye kuta za nyumba zao,wakijua wamemuweka Yesu ndani,kumbe ni sura yake yeye ambaye na yeye anahitaji huruma kutoka kwa Mungu.
"Jamani sikieni narudia tena mimi sio Yesu mimi ni muigizaji tu wa filamu kama walivyo waigizaji wengine na baada ya kumaliza kazi yangu nililipwa ujira wangu nikaendelea na kwenda kucheza filamu nyingine hivyo msiiabudu picha yangu,wengine wanatembea nayo kwenye magari,wengine mmeweka madukani kwenu,niwashauri kama kuomba basi muombeni yule aliye ndani ya mioyo yenu," alisema Brian Deacon ambaye kwa sasa ana umri miaka 79.
Deacon amejaliwa kupata mtoto mmoja tu anayeitwa Lara Parker, kwa mke wake wa kwanza aitwaye Rula Lenska....ambapo alitengana na mkewe huyo na kuoa mke mwingine aitwaye Nathalie Bloch, ambaye alikuwa ni muigizaji na Pruducer kutoka nchini Ufaransa.
Filamu ya Jesus Christ, ambayo mpaka sasa imeangaliwa na watu zaidi ya bilioni tatu huku karibia watu milioni 117,waligeuka na kuwa wa wakristu kweli baada ya kuangalia filamu hiyo,ambapo mpaka sasa imeshatafsiriwa kwa lugha zipatazo 582.
(Picha ya mwisho kabisa inamuonyesha Brian akiwa ameezeka na nyingine za mwanzo akiigiza na nyingine enzi za ujana wake na nyingine akiwa amembeba Yesu akiwa mdogo na Yesu akiwa na umri wa miaka 12 na yeye).