NHIF Watangaza Kurudisha Dawa 178 zilizoondolewa Bima ya Afya


Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umetangaza kurejesha dawa 178 pamoja na kujumuisha dawa nne zilizokuwepo kwenye muongozo wa Taifa wa matibabu lakini hazikuwemo kwenye orodha ya Taifa ya dawa muhimu (NEMLIT) ambazo umezijumuisha dawa hizo kwenye kitita chake cha mafao cha mwaka 2023.

Taarifa kwa umma ya NHIF iliyotolewa na Kaimu Meneja Uhusiano NHIF Grace Michael imesema hatua hiyo inaongeza wigo wa upatikanaji wa dawa kwa Wanachama kwa kuzingatia miongozo ya tiba nchini

Kutokana na maboresho hayo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umewahakikishia Wanachama wake kuwa huduma za matibabu zitaendelea kupatikana katika vituo vyote vilivyosajiliwa Nchi nzima na endapo kutakuwa na changamoto zozote za kiutekelezaji NHIF imetoa wito kwa vituo vyote vinavyotoa huduma za afya nchini viwasiliane na mfuko huo ili kuepuka usumbufu usiokuwa na lazima kwa Wateja wao.

NHIF imesema iwapo Mwanachama yeyote atakutana na changamoto yoyote katika upatikanaji wa huduma ameshauriwa kuwasiliana na mfuko huo kupitia kituo cha huduma kwa wateja kwa kupiga simu bila malipo namba 199.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad