Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa aliyokuwa ameikata Mahakama Kuu kanda ya Arusha dhidi ya Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita, kupinga maamuzi ya rufaa ambayo ilibariki maamuzi ya Mahakama hakimu Mkazi Arusha.
Mahaka ya Hakimu mkazi Arusha iliwaachia huru Ole Sabaya na wenzake sita baada ya kushtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi na kuongoza genge la uhalifu.
Katika Kesi hiyo Sabaya na wenzake walidaiwa kujipatia kiasi cha 90 milioni kutoka kwa Mfanyabiashara Francis Mroso kinyume na sheria.
Akizungumzia uamuazi huo nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Wakili wa Sabaya, Moses Mahuna amesema mteja wake kwa sasa hana kesi nyingine, yupo huru na ana uwezo wa kuwania nafasi zozote za kiuongozi.
Tangu mwaka 2021 Sabaya amekuwa akibiliwa na kesi mbalimbali baada ya kusimamishwa ukuu wa wilaya na Rais Samia Suluhu Hassan ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zilizokuwa zinamkabili.