Oscar Oscar Kuchukuliwa Hatua kwa Vitendo vya Udhalilishaji

 

Oscar Oscar Kuchukuliwa Hatua kwa Vitendo vya Udhalilishaji

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimekemea Vitendo vya Udhalilishaji vinavyofanywa na Mwanahabari Oscar Oscar kupitia habari picha za mzaha (Memes) anazozisambaza Mitandaoni.


LHRC imenukuu Ibara ya 12 ya Katiba ya Tanzania inayolinda heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa Utu wa Mtu na inapinga ubaguzi, Mkataba wa kupinga aina zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake pamoja na Ibara ya 4 ya Mkataba wa Maputo.


Aidha, taarifa ya LHRC imetoa Onyo kwa mwanahabari huyo na kumtaka kuacha mara moja kuweka maudhui ya Udhalilishaji dhidi ya Wanawake ambayo yanafanya waonekane kama chombo cha starehe. Kinyume na hapo LHRC imesema itachukua hatua za Kisheria.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad