Paul Makonda "Ningekuwa na Uwezo Ningeifuta Halmashauri ya Jiji la Arusha"


Paul makonda


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, ameshangazwa na Halmashauri ya jiji kupatiwa Sh bilioni 7.7 na serikali kuu na kutumia sh milioni 500 na miradi ya maendeleo kukwama.

Makonda leo alipatiwa taarifa ya Halmashauri ya jiji la Arusha ambapo waliwashangaa viongozi hao namna wanavyotekeleza majukumu yao na miradi kukwama licha ya fedha kupewa.

"Naibu meya nimejiuliza kwa nini tuna jiji kama miradi yote hiyo ilitakiwa kutekelezwa alafu haijatekelezwa tumebakiza mwezi mmoja na fedha zipo akili yangu ya haraka haraka ingekuwa ni mamlaka yangu ningewafukuza kazi wote,”amesema Makonda na kuongeza kuwa;

“Sio tu kuwafukuza kazi kule Marekani katiba inasema Rais anaweza kutoka madarakani kutokana na afya na mambo mengine hapa nawaza hakuna utaratibu unang’olewa kwenye majukumu yako kwa sababu umeshindwa kutimiza na kushtakiwa kupoteza muda wa wananchi,”

Alisema fedha iliyotumika kutoka serikali kuu ni asilimia 6.4 na miradi ya maendeleo haijatekelezwa licha ya fedha kuwa nazo.

"Ujue nawaza sijui watu wanapataje kazi najiuliza watu wanafanyaje mpaka wanaonekana wamaana jamani..kama ushirikina upo basi hii nchi inayo tukipita katika miradi tutaona hata jengo lao la utawala sijui linaendaje sijui ni kitu gani kinaendelea mmepewa kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo au ya kuonyesha nani mkubwa," amesema Makonda.

Aidha Makonda amekemea tabia ya malumbano na kuvutana kwa watumishi na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha suala ambalo limekuwa likisababisha kukwama kwa miradi mingi ya maendeleo licha ya serikali kutoa fedha.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad