PAUL Makonda: Sitishiki, Nitawapiga Spana, Mkinisema Kama Mnanifanyai Masaji

PAUL Makonda: Sitishiki, Nitawapiga Spana, Mkinisema Kama Mnanifanyai Masaji


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema hatishiki na kauli zinazotolewa dhidi yake kuhusu kumdhalilisha mwanamke ambaye ni mtumishi wa Serikali wilayani Longido mkoani Arusha.


Makonda ametangaza vita kali dhidi ya wazembe na wala rushwa katika Mkoa wa Arusha bila kujali maneno ya watu katika kusimamia utendaji unao zingatia haki.


"Nasikia kuna watu wanaangaika na mitandao yao ile, ni kama wananipigia rhythm wakati wa kulala, mimi kwa umri huu nitishike na kauli za watu? na wanavyotoa hizo kauli mimi nasikia hiyo hali ya kunipa nguvu ya kuendelea na leo nipo Monduli.


“Umoja wa waovu,wazembe na wala rushwa ni mkubwa sana ukimgusa mmoja utaona tu na wengine lazima wajitokeze hapo ndo utajua kumbe na huyu yumo? Niombe mnivumilie,mtapata watu wengine watakao wapetipeti lakini mimi hapana.


“Mkoa wetu hatuta wavumilia watumishi wazembe, hatuwezi kwenda hivyo nitawapiga spana wazembe mpaka wanyooke,”amesema Paul Makonda.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad